MPYASwahiliPOS Kiganjani: duka lako mkononi

Duka lako lote, kwenye kompyuta na mkononi.

Mfumo kamili wa mauzo kwa maduka ya Tanzania: POS ya haraka, madeni, stock, ripoti na risiti. Unafanya kazi hata bila intaneti.

  • Inafanya kazi bila intaneti
  • Kiswahili na English
  • Imetengenezwa Tanzania
Dashibodi ya SwahiliPOS
9:41
SwahiliPOS Kiganjani: mauzo ya leo
Mauzo ya leoTsh 327,900
Madeni yaliyochelewa12 · Tsh 523,450
Bila intanetiInauza kwenye mtandao wa ndani wa duka
Risiti ya printaPrinta ya 80mm, PDF au kushiriki
Malipo yoteCash, M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, benki
Data salamaBackup kwa sekunde, kila badiliko linarekodiwa
Ziara ya mfumo

Hivi ndivyo SwahiliPOS inavyoonekana.

Skrini halisi za mfumo. Chagua sehemu uone.

duka.local/dashboard

    Vipengele

    Kila kitu duka linahitaji, mahali pamoja.

    Kuanzia kuuza kaunta hadi kujua faida ya mwezi, bila daftari wala hesabu za mkono.

    POS ya haraka

    Skani barcode au tafuta kwa jina. Bidhaa ikirudiwa idadi inaongezeka. Simamisha bili, endelea baadaye.

    Madeni bila kuchanganya

    Deni la kila mteja, la zamani na jipya, linaonekana kwenye risiti. Wakumbushe kwa SMS moja.

    Stock na Stoo

    Vipimo vingi (pakiti, katoni, ndoo), stoo tofauti na duka, tahadhari ya bidhaa zinazoisha.

    Ripoti za faida

    Mauzo, faida, matumizi, madeni na stock kwa siku, wiki au mwezi. Pakua Excel au PDF.

    Wauzaji na ruhusa

    Kila muuzaji ana jina, PIN na ruhusa zake. Unajua nani aliuza nini, na lini.

    Backup na Sync

    Hifadhi nakala kwa sekunde. Ukitaka, nakala ya mtandaoni inasawazishwa yenyewe.

    Risiti mahiri · Thermal 80mm

    Mteja anaona deni lake waziwazi. Hakuna ubishi.

    Risiti ya SwahiliPOS inajua kama mteja amelipa taslimu, amekopa, au ana deni la zamani, na inaonyesha kile tu kinachohitajika.

    • 1
      Mteja wa cashJumla Kuu peke yake. Risiti fupi na safi.
    • 2
      Mteja wa mkopoJumla Kuu, kiasi kilicholipwa na deni linalobaki.
    • 3
      Mwenye deni la zamaniDeni la zamani linaongezwa tu kama bado halijalipwa. Lililolipwa halionekani tena.
    Risiti ya mfano ikitoka kwenye printa ya thermal 80mm
    SwahiliPOS · Thermal 80mm
    Printa ya thermal 80mmRisiti inatoka papo hapo baada ya malipo
    SwahiliPOS Kiganjani

    Duka lako, popote ulipo.

    App ya mwenye duka. Ingia kwa PIN, uone mauzo ya leo, madeni na stock kwa wakati halisi, hata ukiwa safarini.

    9:41
    Kiganjani ikifunguka
    Inaunganisha na dukaSync ya mauzo yako
    9:41
    Kuingia kwa PIN
    Ingia kwa PINTarakimu 4, salama na haraka
    9:41
    Nyumbani: mauzo ya leo
    Mauzo ya leoOda, makusanyo na faida
    9:41
    Orodha ya mauzo
    Kila odaNani amelipa, nani anadaiwa
    9:41
    Madeni ya wateja
    Madeni yoteKumbusha kwa SMS moja
    Mauzo kwa wakati halisiCash, mkopo na faida ya leo, wiki na mwezi.
    Madeni yanayochelewaOrodha ya wanaodaiwa, tayari kupiga simu au SMS.
    Stock inayoishaJua bidhaa zinazokaribia kwisha kabla hazijaisha.
    Wauzaji wakoMauzo ya kila muuzaji kwa siku, wiki na mwezi.
    Kuanza

    Unaanza kuuza ndani ya siku moja.

    Tunasakinisha

    Tunaweka SwahiliPOS kwenye kompyuta ya duka na kuunganisha kompyuta, simu na printa za duka.

    Tunahamisha data

    Bidhaa, wateja, mauzo na madeni kutoka mfumo uliokuwa unatumia yanahamia bila kupotea.

    Tunawafundisha

    Wauzaji wanajifunza kwa dakika chache, kwa Kiswahili. Msaada unaendelea kwa WhatsApp.

    Bei

    Chagua kinachofaa duka lako.

    Lipa kila mwezi, au lipa mara moja tu bila ada ya kila mwezi.

    Mwezi · Msingi

    Kwa duka linaloanza na SwahiliPOS.

    Tsh25,000
    kwa mwezi
    • POS, madeni, stock na ripoti
    • Inafanya kazi bila intaneti
    • Msaada kwa WhatsApp
    Chagua mpango
    INAPENDWA ZAIDI

    Mwezi · Pro

    Mfumo kamili pamoja na Kiganjani App.

    Tsh35,000
    kwa mwezi
    • POS, madeni, stock na ripoti
    • Inafanya kazi bila intaneti
    • SwahiliPOS Kiganjani App
    • Msaada kwa WhatsApp
    Chagua mpango

    Leseni ya kudumu

    Lipa mara moja tu. Hakuna ada ya mwezi.

    Tsh1,500,000
    mara moja
    • POS, madeni, stock na ripoti
    • Hakuna ada ya kila mwezi
    • Inasakinishwa kwenye kompyuta ya duka
    Chagua mpango

    Nakala Online + Sync

    Data ya duka lako mtandaoni, inasawazishwa yenyewe. Unaweza kuiongeza kwenye mpango wowote.

    Tsh115,000/ mwaka
    Maswali

    Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

    Je, inahitaji intaneti?

    Hapana. SwahiliPOS inafanya kazi kwenye mtandao wa ndani wa duka bila intaneti. Intaneti inahitajika tu kwa nakala ya mtandaoni na Kiganjani App.

    Inafanya kazi kwenye kompyuta gani?

    Kompyuta moja ya Windows dukani inakuwa seva. Kompyuta nyingine na simu za duka zinaingia kupitia browser.

    Naweza kuhamisha data ya mfumo wangu wa zamani?

    Ndiyo. Tunahamisha wateja, bidhaa, mauzo na madeni kutoka mfumo uliokuwa unatumia.

    Data yangu iko salama?

    Backup inachukua sekunde na kurudisha ni rahisi. Kila mtumiaji ana PIN au nenosiri lake, na kila badiliko linarekodiwa.

    Nikilipa mara moja, nitalipa tena?

    Hapana. Leseni ya kudumu inalipwa mara moja tu. Nakala Online + Sync ni hiari, kwa mwaka.

    Uko tayari kuona SwahiliPOS dukani kwako?

    Tuandikie WhatsApp au utupigie, tukuonyeshe mfumo ukifanya kazi.